na mwandishi we

Chuo kikuu cha taifa zanzibar (suza) leo  (28/03/2024) kimefanya mazungumzo na shirika la serikali uturuki  (tika) ambalo lipo chini ya waziri mkuu wa nchi hiyo ili kujenga uhusiano mwema na kuimarisha sekta ya kilimo. Naibu makamu mkuu wa suza, dk. hashim hamza  chande  anayeshughulikia masuala ya fedha, mipango na utawala alisema fursa  hii imekuja wakati muafaka ambapo suza inaendelea na kutanua wigo wa miundo mbinu yake sambamba na kuongeza idadi ya wanafunzi,a liongeza kuwa suza kupitia chuo cha kilimo kizimbani, kinawapatia utaalamu wa kilimo cha mazao ya chakula, biashara pamoja na ufugaji  wakulima  na wanafunzi.

‘chuo kinawafundisha wakulima wa mpunga kwa makundi mbinu bora za kilimo hicho’’, aliseman aye mkurugenzi mkaazi wa shirika hilo, bibi filz sahinci, alisema  uturuki kupitia mashirika yake mbali mbali ina uzoefu na utaalamu mkubwa katika masuala ya kilimo.

‘’tunataka kujuana shughuli zetu ili tuone fursa  ziko wapi  tuzitumie kwa pamoja, tunajenga marafiki  ambao tunafanya  nao kazi pamoja’’, alisisitiza bibi fili, aidha, aliongeza kuwa tika itatoa fursa ya kuleta  wataalamu wa kilimo na baadaye mafunzo hayo yaendelezwe na wazaw

TIKA ni shirika ambalo limeanzishwa mwaka 1992 nchini uturuki  na kuanza  kazi zake tanzania mwaka 2017   hadi sasa limekamilisha miradi 300  katika sekta zikiwemo ya kilimo, afya, elimu na maji.