SUZA yadhamini  mafunzo watayarishaji wa vipindi

Na Nasima Haji, MWANZA

CHUO Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA)  kimepokeza cheti cha Shukurani kufuatia kudhamini  mkutano wa  mafunzo  wa 108  wa watayarishaji wa vipindi vya  elimu kwa umma  yaliyotolewa na Shirika la Utangazaji  Tanzania (TBC).

Cheti hicho  kimetolewa  na  Waziri wa Habari,  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye kutokana na kuthamini mchango na ushiriki wa maofisa  waliopata mafunzo hayo walioziwakilisha taasisi zao kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambao pia wamechangia  mkutano  huo.

 Katika mafunzo hayo, maofisa wa habari zaidi ya 120 kutoka taasisi za serikali, mashirika ya umma na binafsi ulifayika leo katika hoteli ya Crest, jijini Mwanza.

 Washiriki walijifunza mada kadhaa zikiwemo, mawasiliano ya ushawishi, mawasiliano ya kimkakati, uzalendo katika muktadha wa dhana nne za  uvumilivu  (Reconciliation), ustahamilivu (Resilience),  Ukarabati (Rebuilding), na mageuzi (Reform). Mada nyengine ni matumizi ya mitandao, utayarishaji wa vipindi vya televisheni na redio na upigaji picha.

 Akiwahutubia washiriki wa mafunzo hayo,  Mhe.   Nnauye  aliwahimiza maofisa wa mawasiliano na uhusiano  kupitia kwenye taasisi zao kutumia vyombo vya habari kupeleka  maudhui  yenye mtazamo chanya ambao utaleta mabadiliko kwa jamii.

Aliongeza kuwa vyombo vya habari vina jukumu ya kutoa maoni ya wananchi ili taasisi zinazohusika ziweze  kuyachukua na kuyafanyia kazi.

‘’ Ni matumaini yangu kuwa mkutano huu utaandaa vipindi na taarifa zinazolenga  kutatua kero za wananchi’, alisisitiza.

Mkutano huo wa siku tano ambao ulianza jana na kumalizika siku ya Ijumaa wiki hii na   utawawezesha washiriki hao kutembelea maeneo  ya  vivutio, historia  na miradi ya mikakati.