Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) na Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Fortvalley Cha Marekani vimekubaliana kuanzisha mashirikiano kwenye maeneo ya Kiswahili, Kilimo na Biashara. Hayo yamefikiwa baada ya kikao kilichowakutanisha viongozi wa SUZA wakiongozwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Moh’d Makame Haji na upande wa Fortvalley ukiwakilishwa na Prof. Rayton Sianjema ambapo mashirikiano hayo pia yatakuhusu kuandaa programu za kubadilishana wanafunzi na wanataaluma, utafiti na kusaidia jamii. Kikao hicho kimefanyika leo 8/07/2023, Kampasi ya Tunguu