Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kinawakaribisha wananchi wote kwenye Maonesho yake ya masomo yanayotolewa na Chuo pamoja na udahili wa wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2019/2020 kwa kozi zake mbali mbali za Cheti, Stashahada (Diploma), Shahada ya Kwanza (Bachelor degree), Shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika fani mbalimbali kama vile Ukutubi, Utalii, Ualimu, Kilimo, Afya, Mazingira, Uhasibu na nyingine nyingi.

Maonesho hayo yataaanza siku ya Jumamosi ya tarehe 27 hadi Jumatano ya tarehe 31 Julai, 2019, kuanzia saa 3:00 asubuhi mpaka saa 11:00 jioni, Mnara wa Mapinduzi (Mapinduzi Square), Michenzani.

Maelezo ya kina kuhusu masomo yanayosomeshwa na masuala yote ya udahili (Online Admission) yatafanyika hapo hapo. Ewe mzazi, mlezi, wahitimu wa Kidato cha Nne, cha Sita, Cheti, Stashahada na wananchi wote kwa jumla hii ni nafasi adhimu ya kuijua SUZA na usikubali kuikosa.

WOTE MNAKARIBISHWA