1. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Prof. Said S. Aboud atembelea Banda la SUZA kwenye Maonesho ya 47 ya kimataifa ya Biashara yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Prof. Said akipata maelezo ya mfumo wa ufugaji Smart Poultry Farm ulioandaliwa na Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar. Tembelea kwenye Banda letu namba 57 linalopatikana Jakaya Mrisho Kikwete.