Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dr. Khalid Salum Mohamed ameitaka kamati ya ushauri wa kisekta kufanya kazi kushirikiana kwa pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kwa lengo la kuboresha na utengezaji wa mitaala wenye ujuzi.

Ameyasema hayo wakati akizinduwa kamati ya ushauri wa kisekta katika ukumbi wa Taasisi ya Utalii Kampasi ya Maruhubi, SUZA.

Dr. khalid amesema kushirikiana kwa pamoja kutapelekea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi pamoja na kushauriana juu ya matumizi ya tafiti na uvumbuzi mbali mbali.

Aidha, amefahamisha kwamba chuo hicho kinazidi kusonga mbele kwa kuwa na programu nyingi na kupelekea idadi kubwa ya wanafunzi katika fani mbali mbali.

Nae, makamo mkuu wa Chuo cha SUZA professa Moh’d Makame Haji amefahamisha kuwa kamati hiyo ina jumla ya wajumbe 23 kutoka katika taasisi mbali mbli za serikali na sekta binafsi ,kati ya wajumbe hao wajumbe 11 kutoka ndani ya suza na 12 wametoka nje wa suza.

Chuo cha SUZA ni miongoni mwa vyuo 14 vya wanufaika wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) yaani (Higher Education for Economic Transformation [HEET] project) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia,ambapo Kwa Suza tayari umeshaanza kutekeleza miradi mbali mbali ikiwemo kuwapeleka walimu na wafanyakazi wake njee ya nchi kujiendeleza kitaaluma,sambamba na kununua vifaa mbali mbali YA IT.