Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Prof. Moh’d Makame Haji amesema ujio wa wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi ya Jamii nchini China unaleta faida kubwa kwa Vyuo Vikuu hapa nchini hasa kwa upande wa kitaaluma pamoja nakuimarisha uhusiano ulipo na kutoa nafasi nyingi za kimasomo kwa wafunzi watakaofanya vizuri zaidi. ameyasema hayo maratu baada ya kuhutubia katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa  Taasisi ya Utalii Kampasi ya Maruhubi

Prof. Moh’d  amesema vyuo vikuu pamoja na vyuo  vya amali zanzibar vimefikia makubaliano ya pamoja kwa ajili ya kupata taaluma itakayo saidia  kutambua mali hafi za taifa na kuzitumia ili taifa liweze kujikwamuwa kiuchumi na maendeleo kwa jamii

naye Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa SUZA Dkt. Ali Makame Ussi amesema Chuo hicho cha sayansi ya jamii kina uwelewa mkubwa katika kufanya tafiti mbali mbali na kutatua changamoto katika jamii husika   amesema ipo haja kubwa ya kushirikiana pamoja kubadilishana wataalamu kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar

Kwa upande wake Balozi wa mdogo wa China Zanzibar, Balozi Zhou Yunfan amesema ameridhishwa na uamuzi wa vyuo vikuu kukubali kushirkiana na kubadilishana taluma