Vijana waamshwa  kuuenzi, kuuthamini Muungano

Na Mwandishi Wetu, SUZA

Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) Prof. Mo’hd  Makame  Haji  amewahimiza vijana kuitambua jamii yao  kwa masuala yanayowahusu ili kukabiliana na changamoto zilizoko kwenye jamii.

 Akizungumza katika ufunguzi wa mjadala wa Tathmini  ya miaka 60  ya Muungano wa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA, huko Maruhubi. Prof. haji alisema kwa kufanya hivyo kutawawezesha kuwa na mamuzi muafaka.

‘’Tuendelee kujifunza, tusimame tukijijua sisi ni nani na tukiwa hivyo ndio tutaibua chemchem ya mabadiliko,’’, alisisitiza.

Aliwahimiza vijana kusoma na  kufanya tafiti ili kuujenga Muungano kuwa imara badala ya kuuvunja.

Aliongeza kuwa kizazi cha sasa  kimeikuta hali  tulivu ya   kisiasa na kiuchumi, lakini kuna watu   ambao wamepitia shida kubwa hadi kufikia hapa  ilipo Tanzania.

Aidha aliongeza kuwa amefurahishwa na wazo la kuwakutanisha vyuo  vijana  kutoka Taasisi za Elimu ya Juu)   wanajadili manufaa yaliyopatikana na kubaini changamoto na kuzifanyia kazi.

Akiwasilisha mada kuhusiana na udugu asilia wa Tanzania  na upekee wa Watanzania, Mhe. Balozi Salum Ali, aliwakumbusha   watanzania husussan vijana kufahamu walikotoka  ili waweze kuuenzi na kuuthamini Muungano wa Tanzania.

’’  Leo  mko hapa kwenye vyuo hii ni kwa sababu wazee wetu walijitolea, kwani wengine waliuawa wengine hawajulikani waliko, Tusiwaachie    watu wa nje kuzungumza historia yetu, haizungumzwi  vizuri’’, alisisitiza.

Alifahamisha kuwa  Watanzania wanapaswa  kufahamu walikotoka  ili waweze kuuenzi na kuuthamini Muungano’

Naye Mwanasiasa mkongwe Mhe. Hamad Rashid akichangia mjadala huo alisema kuwa kuna umuhimu wa vijana  kufuatilia na kuufahamu Muungano wa Tanzania ili baadaye waweze kuulezea kwa vizazi vijavyo.

Akiwasilisha mada ya michezo na sanaa, Salim Said Salim ambaye ni mwanahabari na mwanamichezo mashuhuri zanzibar amewahimiza vijana  amewhimiza kusoma  nyanja zote  hasa watoto wa kike kwani bila ya kusoma watakuwa sumu na kuharibu mazuri yaliyopiganiwa kuwepo.

Akizungumzia kuhusu utatuzi wa  kero za Muungano, Dkt Harrison Mwakiembe.  changamoto zikikaa sana bila kuangaliwa zinakuwa tatizo na kwa Muungano wa Tanzania kati ya changmoto 25 zilizokuwepo ni  changamoto nne (4) tu ndizo ambazo hazijatatuliwa.

Katika mjadala huo , mada mbali mbali zilijadiliwa kama vile  ‘Undugu wetu wa Asilia na Upekee wa Muungano’  iliyowasilishwa na Balozi Salum Ali,  Hatua za Utatuzi wa Kero za Muungano na  Dkt Harrisson Mwakiembe,  Faida na Changamoto  za Muugano na Dkt. Idd Mandi, Uhai wa Ndoto za Waasisi wa Muungano ,  ‘Fursa Zilizotolewa na Kurahisishwa na Muugano’  na Maggid Mjengwa, ‘Mapokeo ya Muugano kwa kizazi kipya’ na  Dkt Richard Mbunda na ‘Michezo na Sanaa’ iliwasilishwa na Salim Said Salim   mwanahabari  na mwanamichezo mahiri nchini.

Mjadala huo uliandaliwa kwa ushirikiano baina ya SUZA na Taasisi ya uchambuzi ya Tanzania bara uliwashirikishwa wanafunzi wote wa SUZA.