
Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dr Salum Slim Mohammed ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar SUZA kwa kuendelea kufanya tafiti mbalimbali za Afya ambazo zinasaidia wizara katika kuboresha Afya nchini
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku 3 ya mradi wa Uimarishaji wa Huduma jumuishi za VVU, TB na Malaria wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua kwa baadhi ya wakuu wa vituo vya Afya Unguja na Pemba

Nae Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar Dkt Salma Mahmoud Abdi amesema mradi huu utasaidia kupunguza vifo vya mama na watoto na kusaidia kuzuia msongo wa mawazo kwa wazazi waliojifungua.
Mradi huu umefadhiliwa na Global Fund kwa kushirikiana na Liverpool School of Tropical Medicine cha nchini Uingereza pamoja na Chuo Kikuu Cha Taifa Zanzibar (SUZA).