Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar – SUZA, chaandaa kongamano la kitaaluma

Na Mwandishi Wetu, SUZA

Chuo Kikuu cha taifa Zanzibar (SUZA) kimeandaa kongamano la kitaaluma  likiwa ni sehemu ya shamra shamra za maadhimisho ya miaka sitini (60) ya Mapinduzi  Matukufu ya Zanzibar.

Taarifa iliyotiwa saini na  Makamu Mkuu wa Chuo cha SUZA, Profesa Moh’d Makame Haji imeeleza kuwa kongamano hilo linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 6 Januari, 2024 saa2:00 asubuhi  ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa  kuwa Mhe. Profesa Adolf Faustine Mkenda (Mb) na Waziri waElimu, Sayansi naTeknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi  tarehe 6 Januari, 2024 saa 2:00 asubuhi katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein uliopo Kampasi ya Tunguu Mkoa  wa Kusini Unguja.

Katika kongamano hilo, wanataaluma, wanafunzi, viongozi mbali mbali wastaafu na waliopo madarakani wamealikwa ni Waziri wa   Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman na Mhe. Steven Wasira ambaye hivi sasa ni  Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kipindi cha pili cha pili cha miaka minne,    Balozi Mohamed Ramia, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud na  Ndg. Abdulla Mzee Abdulla, Katibu Mkuu Mstaafu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.

Kongamano hilo linabeba  kauli mbiu ‘Tuimarishe Uchumi, Uzalendo na Amani kwa Maendeleo ya Taifa Letu’.