Sura mpya SUZA, Tunguu yaja
Na Nasima Haji, SUZA
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Profesa
Moh’d Makame Haji, amesema Chuo kipo katika mchakato wa
mabadiliko ya miundombinu kwa kuandaa mpango mkuu wa mageuzi wa
utanuzi wa SUZA wa miaka 20 ijayo.
Alisema mpango huo utaongeza nguvu ya kufanya kazi na kwenda
sambamba na mabadiliko na kufkia matumaini ya viongozi wakuu wa
nchi ya kutaka kuona taasisi zinafanya kazi kwa ufanisi na zinaleta
manufaa wakati huu hapo baadaye.
Akizungumza katika kikao maalum cha kupitia sera ya mawasiliano,
Profesa Moh’d alisema Chuo kitajenga majengo ya kisasa ambayo yatatoa
fursa ya kutumiwa na wataalamu, wanafunzi na wadau wengine wa
elimu.
Aliitaja miradi ambayo inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa ni Mradi wa
wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi  (HEET) ambao utajenga
majengo ya kisasa ikiwa ni pamoja na maabara kubwa ya kisasa na
dakhalia za wanafunzi wa kike na wa kiume na skuli ya kilimo.
Alifahamisha kuwa mradi mwengine unaofadhiliwa na Benki ya
Maendeleo ya Afrika (BADEA) ambapo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inawekeza asilimia 10 ya mradi huo ni wa kujenga majengo mbalimbali
ikiwa ni pamoja na viwanja vya michezo.
Vile vile, Profesa Makame alisema kwa vile SUZA inashiriki  katika sekta
ya michezo hivyo, Chuo kitajenga  viwanja vya michezo  vyenye viwango
cha Olimpiki, nyumba za  makaazi  za walimu na wafanyakazi na  viongozi
wakuu wa Chuo.
Aidha, kutakuwepo  na kumbi za kisasa  na kutoa huduma mbalimbali
kama vile maegesho, sehemu za kupata huduma za chakula na maduka
makubwa ambayo pia yatakodishwa.
‘’ Hadi tukimaliza tutakuwa tumejenga majengo 39 ambapo skuli zote
zilizo chini ya Chuo  na nyengine  ambazo hazijaanzishwa lakini zimetajwa
pia zitajengwa.’’ Alifahamisha.
Aliwahimiza wadau kutoa ushirikiano mkubwa kwa kila mmoja kuwa
sehemu ya chuo ili kutoa mwelekeo wa kule chuo kinakotaka kwenda.

Tunataka kutengenza Chuo chenye ubora, dira na matarajio yetu kuwa
Chuo cha ubora wa kipekee wa kutoa taaluma katika ukanda wa Afrika ya
mashariki na nje ya Afrika.
Mwaka jana SUZA iliingia katika vyuo vikuu bora barani Afrika
vilivyochaguliwa kutokana na ubora wa kazi vinavyofanya kwa kushika
nafasi ya 157 kati ya vyuo 200.
‘’Hii si nafasi ndogo ikilinganishwa na vyuo vikuu vilivyoko Barani Afrika
1,274,’’ alisema

 

mwisho