KUMBUKUMBU YA MIAKA 23 YA KIFO CHA RAIS WA KWANZA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

14 OKTOBA, 1999 – 14 OKTOBA, 2022


Baraza la Chuo, Menejimenti na Wanajumuiya wote wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar inaungana na watanzania na waafrika  kwa ujumla katika maadhimisho ya kumbukumbu za miaka 23 ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Daima ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuikomboa Tanzania na Afrika ambapo mpaka sasa bado maono yake yanaendelea kusihi ya kuitaka Tanznaia kuwa nchi yenye umoja, amani na mshikamano. Aidha Chuo kinaahidi kuyaenzi na kutekeleza falsafa zake kivitendo katika kuleta ustawi wa wananchi kijamii na kiuchumi.

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kinaahidi kuendeleza juhudi za kutimiza wajibu wake wa kuchangia maendeleo ya elimu nchini na kuleta mabadiliko ya kiuchumi  na  kijamii kupitia utoaji wa elimu bora.

Kwa taarifa zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar tembelea tovuti  http:// www.suza.ac.tz


Mawasiliano yote rasmi na Chuo yafanywe kupitia kwa:

Makamu Mkuu wa Chuo

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar

Sanduku la Posta 146

Zanzibar, Tanzania

Barua pepe: vc@suza.ac.tz