CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)
Sanduku la Posta 146, Zanzibar- Tanzania
Tovuti: http://www.suza.ac.tz Barua pepe: vc@suza.ac.tz
Kichocheo cha Mabadiliko ya Jamii
SALAMU ZA KUMBUKIZI YA KIFO CHA RAIS WA KWANZA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KUMBUKUMBU YA MIAKA 24 YA KIFO CHA RAIS WA KWANZA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAYATI MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE
14 OKTOBA, 1999 – 14 OKTOBA, 2023
Baraza la Chuo, Menejimenti na Wanajumuiya wote wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar inaungana na watanzania na waafrika kwa ujumla katika maadhimisho ya kumbukumbu za miaka 24 ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Daima ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa wa kuikomboa Tanzania na Afrika ambapo mpaka sasa bado maono yake yanaendelea kusihi ya kuitaka Tanzania kuwa nchi yenye umoja, amani na mshikamano. Aidha Chuo kinaahidi kuyaenzi na kutekeleza falsafa zake kivitendo katika kuleta ustawi wa wananchi kijamii na kiuchumi.
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kinaahidi kuendeleza juhudi za kutimiza wajibu wake wa kuchangia maendeleo ya elimu nchini na kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kupitia utoaji wa elimu bora.
Kwa taarifa zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar tembelea tovuti http:// www.suza.ac.tz
Mawasiliano yote rasmi na Chuo yafanywe kupitia kwa:
Makamu Mkuu wa Chuo
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
Sanduku la Posta 146
Zanzibar, Tanzania
Barua pepe: vc@suza.ac.tz