RASIMU ZA SERA YA JINSIA NA SERA YA UDHALILISHAJI YAJADILIWA SUZA
Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA kimesema kinatarajia kuanzisha Dawati la jinsia ili kuweka mazingira salama ya kusomea kwa Wanafunzi wa jinsia zote mbili .
Kauli hiyo imetolewa na Makamu mkuu wa Chuo cha Taifa Zanzibar SUZA Prof.Moh’d Makame Haji wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa kupitia Rasimu za Sera ya Jinsia na Sera ya Kupambana na Udhalilishaji wa Kijinsia kupitia Mradi wa Higher education for Economic Transformation Project (HEET).
Amesema Mradi huu unagharimu dola za kimarekani 425 milion. Ambapo SUZA imepangiwa kutumia dola za kimarekani milioni 20 hadi kukamilika kwake na unatarajiwa kusaidia taasisi za Elimu ya juu kutanua na kuboresha majengo na kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia, kupitia mitaala na kutengeneza mitaala mpya, kuboresha miundombinu ya ICT na kusomesha walimu.
Nae Mkuu wa Idara ya Sayansi Jamii ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA Bw.Abdulrahman Mustafa Nahoda amesema kuwa kuwepo kwa Dawati la kijinsia ni Muhimu kwa ajili ya kushughulikia matatizo ,pamoja na kuyatolea ufumbuzi kwa jamii na kupelekea kupunguwa maswala ya Udhalilishaji.