CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)

TAARIFA KWA UMMA

Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kinapenda kuutaarifu umma kuwa, kimetoa orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa ngazi ya cheti, Stashahada (Diploma) na Shahada ya kwanza (Bachelor degree) kwa mwaka wa masomo 2021/2022 kwa programu mbali mbali. Waombaji wote waliochaguliwa wanatakiwa waingie kwenye akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba kwa lengo la kupata barua za udahili (admission letter) pamoja na mambo mengine muhimu ya kujiunga na Chuo.

Aidha kwa wale ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kwa awamu ya kwanza, waombe kozi nyengine zilizotangazwa na chuo kwa awamu ya pili inayotarajiwa kufunguliwa tarehe 24/08/2021 na kufungwa tarehe 06/08/2021. Kwa taarifa zaidi na orodha ya majina ya waliochaguliwa tembelea website yetu www.suza.ac.tz .

Uongozi wa Chuo unawaomba waombaji wote ambao wanapata changamoto zozote katika kwenye mfumo wa uombaji wasisite kuwasiliana na maafisa udahili katika kampasi tofauti za chuo kwa ajili ya kupata msaada zaidi.

Imetolewa na Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri

Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar

Tangazo la waliochaguliwa …