Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kinawakaribisha wanachi wote kwenye maonesho yake ya masomo yanayotolewa na Chuo pamoja na udahili wa wanafunzi wapya kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kwa kozi zake mbali mbali za cheti, stashahada (diploma), shahada ya kwanza (Bachelor degree), Shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada ya Uzamivu (PhD).

Maonesho hayo yataaanza siku ya Jumamosi ya tarehe 28-31 Julai, 2018, kuanzia saa 3:00 mpaka saa 11:00 Jioni, Mnara wa Mapinduzi (Mapinduzi Square) Michenzani.

Maelezo ya kina kuhusu masomo yanayofundishwa na masuala yote ya udahili (Online Admission) yatafanyika hapo hapo. Ewe mzazi, mlezi, wahitimu wa kidato cha nne na cha sita na wananchi wote kwa jumla hii ni nafasi adhimu ya kuijua SUZA na usikubali kuikosa.

WOTE MNAKARIBISHWA