TANGAZO LA MAHAFALI YA 18 YA CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA

ZANZIBAR (SUZA)

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kinawatangazia wahitimu wote wa mwaka wa masomo wa 2021/2022 wa Kampasi zote pamoja na wananchi wote kwa jumla kwamba, mahafali ya 18 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar yatafanyika siku ya jumatano tarehe 28 Disemba, 2022 katika ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein ulioko Kampasi ya Tunguu kuanzia 2:30 asubuhi.

Mazoezi ya mahafali (rehearsal) yatafanyika Jumanne tarehe 27 Disemba, 2022 kuanzia saa 2:30 za asubuhi katika eneo yatakapofanyika mahafali hayo. Wahitimu wote watakaoshiriki katika mahafali ni lazima washiriki katika mazoezi haya katika siku na wakati uliotajwa.

Aidha wahitimu watalazimika kuthibitisha ushiriki wao katika kampasi ya tunguu kuanzia siku ya ijumaa tarehe 23 Disemba, 2022 na uthibitisho huo uambatane na malipo ya joho la mahafali kwa kutumia namba ya malipo (control number) ambazo zitatolewa kupitia ofisi za wahasibu na baada ya malipo wawasilishe ankara ya malipo kwa ajili ya uhakiki.

Majoho ya mahafali yatatolewa katika Kampasi ya Tunguu kuanzia siku ya Ijumaa ya tarehe 23 Disemba, 2022 saa 3.00 za asubuhi hadi saa za 10.00 Alasiri na mwisho wa kutolewa ni siku ya mazoezi ya mahafali. Malipo ya kukodi joho ni Tsh. 25,000/- ambazo zitalipwa kupitia akaunti ya SUZA ya Benki ya Watu wa Zanzibar ama wakala wa PBZ.

Wahitimu wanapaswa kurudisha majoho si zaidi ya tarehe 2 Januari 2023. Faini ya TZS. 5,000 itatozwa kwa kila siku itakayozidi baada ya siku ya mwisho iliyopangwa. Inasisitizwa kuwa wahitimu watajigharamia wenyewe gharama za chakula na malazi kipindi chote cha maandalizi na mahafali. Mtu yoyote hataruhusiwa kuingia kwenye ukumbi wa mahafali baada ya kuingia mheshimiwa mkuu wa chuo. Aidha washiriki wanatakiwa wawe wamekaa ifikapo saa 2.30 asubuhi.

WANANCHI WOTE MNAALIKWA KUSHIRIKI NA KILA ATAKAYESIKIA TANGAZO HILI ANAOMBWA AMUARIFU MWENZIWE

IMETOLEWA NA OFISI YA NAIBU MAKAMU MKUU WA CHUO – TAALUMA, UTAFITI NA USHAURI ELEKEZI