CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)

TANGAZO KWA WAOMBAJI WALIOCHAGULIWA AWAMU YA KWANZA MWAKA 2022/2023

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kinapenda kuutaarifu umma kuwa kimetoa orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo katika ngazi ya Astashahada (Cheti), Stashahada (Diploma) na Shahada ya Kwanza (Degree) kwa mwaka wa masomo 2022/2023 kwa program mbalimbali kama zinavyojionesha hapo chini.

Chuo pia kinapenda kuwataarifu waombaji wote waliochaguliwa kuwa, wahakikishe wanaingia katika akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba chuo kwa lengo la kupata barua za udahili (Admission Letter) pamoja na mambo mengine muhimu ya kujiunga na chuo.

Kwa waombaji wa Shahada ya Kwanza (Degree) ambao wamechaguliwa chuo zaidi ya kimoja (Multiple Selection), wanashauriwa kuingia katika akaunti zao na kuthibitisha (Confirmation) kwa kutumia nambari ya siri (Confirmation Code) ambayo wamerushiwa na TCU kupitia nambari zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wakiomba chuo. Kama bado hujatumiwa nambari ya siri, ingia kwenye akaunti na uiombe kupitia sehemu iliyoandikwa Request Confirmation Code. Tarehe ya wisho ya kufanya uthibitisho huo (Confirmation) ni tarehe 6 septemba 2022.

Aidha chuo kinawataarifu wale wote ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kwa awamu ya kwanza, waombe kozi nyengine ambazo wana sifa nazo zilizotangazwa na chuo kwa awamu ya pili itakayoanza tarehe 24/08/2022 hadi 06/09/2022. Kozi zitakazotangazwa kwa awamu ya pili zimeambatanishwa katika tangazo hili.

Mwisho kabisa, Chuo kinawaomba waombaji wote wasisite kuwasiliana na maafisa udahili katika kampasi tafauti za chuo kwa msaada zaidi.

SENSA KWA MAENDELEO, JIANDAE KUHESABIWA