CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)

TAARIFA KWA UMMA

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), kinapenda kuutaarifu umma kuwa

kimetoa orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo kwa ngazi ya

Shahada ya Kwanza (degree) kwa mwaka wa masomo 2021/2022 kwa programu

mbalimbali. Waombaji wote waliochaguliwa kuwa, wahakikishe wanaingia

katika akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba chuo kwa lengo la kupata

barua za udahili (admission letter) pamoja na mambo mengine muhimu ya

kujiunga na chuo.

Kwa waombaji waliochaguliwa chuo zaidi ya kimoja (multiple selection),

wanashauriwa kuingia katika akaunti zao na kuthibitisha (confirmation) kwa

kutumia nambari ya siri (confirmation code) ambayo wamerushiwa na TCU

kupitia nambari zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wakiomba Chuo.

Kama bado hujatumiwa nambari ya siri, ingia kwenye akaunti na uiombe kupitia

sehemu iliyoandikwa request confirmation code.

Aidha Chuo kinawaarifu wale wote ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa kwa

awamu ya kwanza, waombe kozi nyengine zilizotangazwa na Chuo kwa awamu

ya pili inayotarajiwa kufunguliwa tarehe 24/08/2021 na kufungwa tarehe

06/09/2021. Kozi zinazotolewa awamu ya pili zimeambatanishwa katika tangazo

hili.

Mwisho kabisa, Chuo kinawaomba waombaji wote wasisite kuwasiliana na

maafisa udahili katika kampasi tofauti za Chuo kwa msaada zaidi.