CHUO KIKUU CHA TAIFA CHA ZANZIBAR (SUZA)

Kichocheo cha Maendeleo ya Jamii

SALAMU ZA PONGEZI ZA KUTIMIZA MIAKA 61
UHURU: 9 DISEMBA, 1961 – 9 DISEMBA, 2022

Baraza la Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kwa niaba ya Menejimenti ya
Chuo na Wanajamii wote wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA),
linatoa salamu za pongezi kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa wananchi wote wa
Tanzania kwa kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika. Aidha Chuo
kinajumuika na Watanzania wote katika kusherehekea siku hii adhimu.
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kinafarijika kupokea miongozo kwa ajili
ya uimarishaji wa Chuo na kinaahidi kuendeleza juhudi za kutimiza wajibu
wake wa kuchangia maendeleo ya elimu nchini na kuleta mabadiliko ya
kiuchumi na kijamii kupitia utoaji wa elimu bora.

“ Miaka 61 ya Uhuru, Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu”

—————-

Kwa taarifa zaidi kuhusu Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar tembelea
tovuti

http:// www.suza.ac.tz
Mawasiliano yote rasmi na Chuo yafanywe kupitia kwa:
Makamu Mkuu wa Chuo
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
Sanduku la Posta 146
Zanzibar, Tanzania
Barua pepe: vc@suza.ac.tz