Mwenyekiti wa baraza la Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar SUZA Bi Hamida Ahmed Mohammed akiwaongoza wajumbe wa kamati ya Baraza kwenye kikao cha pamoja na wasimamizi wa miradi mbalimbali inayoendeshwa ndani ya Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kwenye Ukumbi wa mikutano Kampasi ya Tunguu.

Lengo kuu la vikao hivyo, baraza likiwa ni chombo cha maamuzi ya masuala mbalimbali ya chuo kupata taarifa, changamoto ili kuweza kuharakisha utekelezaji.

Vikao hivyo vimeanza tarehe 3/04/2023 na vitaendelea mpaka tarehe 4/04/2023 kwa wajumbe wa kamati ya Baraza kukutana na wasimamizi wa miradi.