Makatibu mahsusi na sekreteriet wa vikao mbalimbali wa chuo kikuu cha taifa cha Zanzibar (SUZA) wapatiwa mafunzo ya Uandaaji wa Mikutano, Ripoti, Uandishi na Utunzaji wa Kumbukumbu za vikao kwa lengo la kuongeza ufanisi kwanye utendaji kazi cha chuo. Mafunzo hayo ya siku tano yametolewa na Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania ambapo yamefanyika kwenye Ukumbi wao uliopo kwenye kituo cha GLC. Aidha mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa HEET ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa Chuo.