Meneja wa Uchumi wa Buluu wa Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB), Captain Hamad Hamad, amekutana na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) kwa ufuatiliaji wa shughuli za SUZA katika mikakati yake ya uanzishwaji wa Tasisi ya Mafunzo ya Bahari. SUZA inakamilisha matayarisho ya mwisho ya ujenzi wa Taasisi ya Mafunzo ya Bahari yatakayojumuisha mafunzo ya ubaharia, matumizi ya vyombo vya bahari kwa ngazi mbalimbali. Ujenzi wa taasisi hiyo unatarajiwa kuanza mapema mwaka huu 2023. Hatua hio ni moja kati ya mikakati ya SUZA kuongeza nguvu sera ya uchumi wa buluu kuwa na nguvu kazi yenye utaalamu unaohitajika.