Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar – SUZA Prof. Moh’d Makamwe Haji amewataka watafiti na wananchi kufanya kazi kwa uweledi ili kupata takwimu sahihi kuhusiana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Ameyasema hayo wakati akifungua warsha ya siku moja ya uzinduzi wa mradi wa “Himili Pamoja” Jinsia na Mabadiliko ya Tabia nchini Tanzania katika hoteli ya Madinatul Bahri ya Zanzibar.

Mradi huu wa muda wa miaka mitano(5) unafadhiliwa na Danida na Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark Kupitia Chupo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar – SUZA, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM na Chuo cha Copenhagen nchini Denmark.