Jamii iendeleze jitihada matokeo ya utafiti- Dkt. Hashim

Na Nasima Haji, SUZA

Wananchi wamehimizwa  kuthamini  kazi zinazofanywa na watafiti zinazolenga kuendeleza utalii wa mazingira kuwa endelevu ili kuigeuza Zanzibar kuwa kivutio cha wageni na wakaazi wake.

Akizungumza katika semina ya kutoa matokeo ya utafiti wa namna gani mazingira yanaweza kuimarisha utalii nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya  Verde Maruhubi leo 31/01/2024.

Naibu Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu chaTaifa cha Zanzibar  (SUZA) Dk. Hashim  Hamza Chande, alisema utafiti umewashirikisha wananchi wa vijiji kwenye maeneo yenye hoteli za kitalii ili kutoa msukumo wa utekelezaji wa matokeo hayo na kupata suluhisho la kudumu.

Alisema kuwa mpango huu miongoni mambo mengine umetoa muongozo wa namna ya kujikinga na mbu kwa njia salama bila kutumia kemikali ambao kwa sehemu kubwa wanazalishwa katika taka na sehemu nyengine zenye uchafu.

‘’Jamii imeshirikishwa katika hatua mbalimbali inafaa ifikirie namna gani wanaweza kufaidika mradi huu endelevu’’, alisema Dk. Hashim.

Aliongeza  kuwa mradi huu unakwenda sambamba na malengo ya dira ya 2050 ya uhifadhi wa mazingira na hivyo kuna uhusiano mkubwa baina ya wawekezaji, wasimamizi kwenye hoteli pamoja na  jamii kusimamia ustawi wa mazingira.

Akizungumza kuhusiana na haja ya kuwa utalii endelevu, Anne Remmen alisisitiza kuwa  kuna umuhimu wa kutoa taaluma kwa kizazi kipya  ili kuendeleza mpango huu  na wengine kuwa mfano  bora wa kutekeleza mipango iliyowekwa.

‘’Mambo ya msingi ya kuufanya utalii wa mazingira kuwa kuzikuwa taka kama fursa, kupunguza uzalishaji lakini pia kuzichakata’’, alisema Anne Remmen.

Naye Mkurugenzi msimamzi wa shughuli za utalii, Adil George kutoka Kamisheni ya utalii akiwasilisha mada kuhusu Kampeni ya Kijani Zanzibar alisema hoteli za kitalii zinazalisha asilimia 60 ya taka zikiwemo za vyakula  ambazo ni muhimu kwa matumizi ya mbolea  lakini pia taka za plastiki zinatumika kutengenezea bidhaa za maatumizi ikiwa ni pamoja na mapambo.

Sheha wa shehia ya Nungwi Bandakuu, Haji Khamis Haji alikiri kuwa tangu ulipoanzishwa mradi huu wameshirikishwa  hata hivyo wanakabiliwa na changamoto ya baadhi ya wananchi  kutofuata maagizo yanayotolewa  hali inayoviza ukuaji wa utalii.

‘’Aliongeza kuwa hakuna utalii  penye uchafu, utalii ndio unatuweka tuiishi maisha ya kupata kipato tunachokitafuta’’ alisema.

Aidha, mafunzo ya kujenga uelewa kuhusiana na masiuala   yanaendelea kutolewa kwa wanavijiji wa Michamvi, Paje na Nungwi kwa ushirikiano na masheha na viongozi wa wilaya.

Utafiti wa EnSuza umewajengea uwezo  walimu watatu kwa ambao wamepata ufadhili  wa masomo katika ngazi ya Uzamivu na Shirika la  Maendeleo la Danida la Denmark  ulianza mwaka 2018 na kusita kutokana na  kuibuka ugonjwa wa COVID19  mwaka 2020- 2021  na baadaye kuendelea hadi kufungwa utafiti huo mwaka huu.

Mradi huu umetekelezwa na  Chuo vikuu vya SUZA ikiwa ndio makao makuu ya mradi  kwa kushirikiana na  Chuo kikuu Huria Tanzania na Wizara ya Afya Zanzibar  na kwa upande wa Denmark ni Chuo Kikuu cha Copenhagen, Chuo Kiku cha Alborg na  Skuli  ya Biashara Copenhagen.