When:
January 17, 2021 all-day
2021-01-17T00:00:00+03:00
2021-01-18T00:00:00+03:00
Where:
Taasisi ya Utalii - Maruhubi

Katika kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Husein Ali Mwinyi katika kukuza uchumi wa buluu, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kinawaalika wananchi wote katika Shindano la vipaji juu ya ubunifu wa kutatua changamoto katika jamii. Shindano hilo litashirikisha wanafunzi wa kampasi zote za SUZA.

Mada: Utalii na Korona (COVID-19)
Mahali: Taasisi ya Utalii – Maruhubi
Siku: Jumapili 17/01/2021
Muda: Saa 3:00 kamili asubuhi
Mgeni Rasmi: Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mh: Lela Muhammed Mussa

Shime kufika kwa wingi ili kujionea vipaji vya wanafunzi wetu. Nyote Mnakaribishwa.
Ahsanteni