Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) na Chuo cha Utalii Cha Taifa vyaimarisha Ushirikiano

Dar es Salaamr, Tanzania – 16 Mei 2024 – Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA) na Chuo cha Utalii Cha Taifa (NCT) leo wametia saini Hati ya Mashirikiano katika hatua ya kipekee ya kuimarisha ushirikiano baina ya taasisi hizi mbili zenye sifa katika elimu ya juu nchini Tanzania.

Hafla hii ya kihistoria ilifanyika katika Kampasi ya Bistani ya Chuo cha Utalii cha Taifa Jijini Dar es Salaam, ikishuhudia kuunganishwa kwa nguvu za taasisi hizi mbili kwa ajili ya kukuza sekta ya utalii nchini Tanzania.
Mkuu wa Chuo cha Utalii cha Taifa, Dk. Florian Mtei, ulifungua ghafla hio kwa hotuba akielezea furaha ya NCT kushirikiana na SUZA katika kufungua milango mipya ya ushirikiano wenye tija katika sekta ya utalii. Aliainisha malengo makuu ya ushirikiano huo,. Maeneo kumi na moja ya mashirikiano yamejumuishwa katika hati hiyo yakiwemo:
• Kubadilishana uzoefu wa kitaalamu baina ya walimu na wanafunzi
• Kushirikiana katika kuandaa programu za kitaaluma
• Kuandaa makongamano na warsha za kubadilishana maarifa
• Kufanya tafiti za pamoja zenye tija
• Kuandaa miradi mbalimbali ya kuimarisha taaluma ya utalii na ukarimu
• Kushirikiana katika usimamizi wa matukio ya utalii

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar, Profesa Moh’d Makame Haji, alionyesha shukrani zake za dhati kwa uongozi wa Chuo cha Utalii cha Taifa kwa kukubali kuanzisha ushirikiano huu muhimu. Alisisitiza umuhimu wa sekta ya utalii kama mchango mkubwa katika uchumi wa taifa na jukumu muhimu la taasisi za elimu katika kuandaa wataalamu bora wa sekta hii. Alisema “hatua hii ni miongoni mwa jituhada za taasisi za elimu nchini za kuunga mkono juhudi za serikali zote mbili, ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibat, za kuimarisha sekta ya elimu chini ikiwemo utekelezaji wa sera ya uchumi wa buluu kwa maendeleo ya kiuchumi.

Akitoa neno la shukurani baada ya utiaji saini wa hati ya ushirikiano, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utalii ya SUZA, Dk. Sharia, alisisitiza kuwa ushirikiano huu wa taasisi hizi mbili unaashiria hatua mpya ya kuimarisha mahusiano yaliyopo na kuimarisha ushirikiano kwa karibu zaidi katika kukuza sekta ya utalii Tanzania.
Hafla hii ya utiaji saini wa Hati ya Mashirikiano imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya SUZA na NCT, ukiashiria dhamira ya dhati ya taasisi hizi mbili katika kukuza elimu bora ya utalii, kuboresha huduma za utalii nchini, na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa ujumla.

Ushirikiano huu unatarajiwa kuleta matokeo chanya kadhaa, ikiwemo: Kuimarisha ubora wa elimu ya utalii Tanzania, Kuongeza ujuzi na uwezo wa wataalamu wa utalii, Kuboresha huduma za utalii zinazotolewa nchini, Kuhamasisha utafiti na maendeleo katika sekta ya utalii, Kuchangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kupitia utalii.