The president visits SUZA
SUZA imetia saini mkataba wa mashirikiano baina yake na Chuo Kikuu cha Indiana kupitia kituo chake cha Swahili Flagship Program huko nchini Marekani.

Hii imetokea ikiwa ni katika hatua za kwanza za kulifanyia kazi agizo la Mkuu wa Chuo na Raisi wa Zanzibar alilolitoa kwenye hotuba yake ya siku ya Mahafali ya kuifanya SUZA kuwa kitovu vha kiswahili kama ilivyo Oxford kwa lugha ya Kiengereza Prof.Rai amesema kufikia adhma hiyo ni suala linalowezekana sana hasa kwa kuzingatia kuwa Kiswahili kinachozungumzwa Zanzibar ni Kiswahili fasaha kuliko maeneo mengine yote Afrika ya Mashariki na Maeneo mengine duniani.

Makamu Mkuu huyo alisema kuwa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kina azma ya kuanzisha Kituo ambacho kitakuwa ni cha kipekee Ulimwenguni kote katika kuendeleza na kukikuza Kiswahili, ambacho pia kitatoa huduma za kufundisha Kiswahili na huduma za tafsiri ya lugha nyengine kwa kiswahili.

Alisema makubaliano hayo kati ya Chuo cha SUZA na Kituo cha Swahili Flagship cha Indiana yataweza kutoa fursa ya kuendeleza programu mbali mbali za Lugha ya Kiswahili kwa mashirikiano baina ya Skuli ya Kiswahili na Lugha za Kigeni na kituo hicho cha Chuo Kikuu cha Indiana Cha Marekani.

Makubaliano hayo yatatoa fursa kwa wakufunzi wa SUZA kusomesha lugha ya Kiswahili katika Kituo cha Flagship cha Kiswahili na pia wao kupata fursa za kujiendeleza kwa kiwango cha digirii ya uzamili katika chuo Kikuu cha Indiana cha Marekani. Pia, katika Makubaliano hayo kutakua na msingi wa mabadilishano ya vifaa mbali mbali vya kusomeshea baina ya Vyuo Vikuu hivi viwili, kama vile CDs, VHF, Audio, Vitabu na kadhalika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo cha Swahili Flagship Dk. Alwiya Omar alisema makubaliano hayo ni msingi muhimu wa mashirikiano, udugu na urafiki baina ya Taasisi hizo mbili katika shughuli mbali mbali za kitaaluma na uendeshaji. Alisema SUZA itarajie kupokea wanafunzi wengi zaidi watakaokuja kujifunza Lugha ya Kiswahili pamoja na utamaduni wa Kizanzibari kwa kuishi pamoja na familia za wazanzibari.

Makamu Mkuu wa Chuo pia alisema kuwa kwa sasa wakati umefika kwa Wazanzibari hususani wasomi walioko nje ya nchi kurudi Zanzibar na kuelekeza nguvu zao katika kuendeleza gurudumu la maendeleo kwa kupitia SUZA.
Photo Gallery
SUZA in Media
OpenAccess
Career@SUZA
Drop Down Menu