Loading Events

« All Events

Sherehe za mahafali ya kumi na mbili (12)

January 21

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar kina furaha kuwatangazia wahitimu na wananchi wote kuwa kitafanya Mahafali yake ya Kumi na mbili (12) siku ya Jumamosi ya tarehe 21 Januari, 2017 katika Kampasi ya Tunguu kuanzia saa 3.00 za asubuhi.

Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ndiye Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar atatunuku vyeti, stashahada na shahada kwa wahitimu wa mwaka wa masomo wa 2015/2016 waliofuzu masomo yao na kustahiki tunuku hizo. Aidha atatoa zawadi kwa mwanafunzi bora wa jumla na wanafunzi wengine katika kozi mbali mbali.

Ushiriki katika Mahafali

  • Wahitimu wote wanashauriwa kuhudhuria katika Mahafali haya na kushuhudia mafanikio yao kielimu. Wote watakaoshiriki wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao si zaidi ya Jumanne ya tarehe 10 Januari, 2017 ambapo watatakiwa kulipia shilingi ishirini na tano elfu (25,000/-) kwa joho na shilingi ishirini elfu (20,000/-) kwa cheti cha kumalizia masomo ambacho kitatolewa siku hiyo hiyo ya mahafali kwa watakaothibitisha na kushiriki katika sherehe hizo.
  • Inasisitizwa kuwa vyeti havitotolewa siku ya mahafali kwa wahitimu watakaoshindwa kuthibitisha ushiriki wao na badala yake watapangiwa siku nyingine za uchukuaji vyeti hivyo hata kama watajitokeza siku ya mahafali.
  • Wahitimu wanatakiwa kufanya malipo ya fedha hizo kupitia Benki ya Watu wa Zanzibar kwenye Akaunti Namba Karatasi za uthibitisho wa malipo kutoka Benki zinatakiwa kuwasilishwa kwa Mkuu wa Idara ya Fedha wa SUZA aliyeko Kampasi ya Tunguu kwa kutoa risiti ya malipo, na kwa Wahitimu walioko Pemba wanaweza kuonesha uthibitisho huo kwa Ofisa wa Idara ya Taaluma na Viwango (DAQA) aliyeko Kampasi ya SUZA ya Benjamin Mkapa, Mchangamdogo, Pemba kwa usajili wa kushiriki na baadae uthibitisho huo uwasilishwe pia kwa Mkuu wa Idara ya Fedha wa SUZA kwa kupatiwa risiti ambayo pia itaoneshwa kwa maafisa wa Kitengo cha Uhusiano kwa usajili rasmi wa ushiriki.

Risiti za malipo ni lazima zioneshwe tena siku ya uchukuaji magauni ya Mahafali.

  • Ushiriki katika mazoezi ya Mahafali ambayo yatafanyika siku ya Alhamisi tarehe 19 Januari, 2017 saa 3.00 za asubuhi ni lazima kwa Wahitimu wote watakaoshiriki. Watakaokosa kushiriki mazoezi hawatoruhusiwa kuingia katika Mahafali na majina yao hayatotajwa miongoni mwa washiriki.
  • Magauni yataanza kutolewa kuanzia Jumatatu ya tarehe 16 Januari, 2017 kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 9.00 za mchana.
  • Wananchi wote wanakaribishwa kushiriki katika Sherehe hizi za Mahafali.

Tangazo limetolewa na:

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo – Taaluma, Utafiti na Ushauri

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar

 

Details

Date:
January 21

Organizer

The State University of Zanzibar
Website:
www.suza.ac.tz

Venue

Main Campus
Tunguu
zanzibar, Tanzania 255 Tanzania, United Republic Of
+ Google Map
Website:
www.suza.ac.tz